Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Kamati za ujenzi simamieni ujenzi kwa ukamilifu

Advertisement Scroll To Keep Reading

 

Na Tegemeo Kastus

Advertisement Scroll To Keep Reading

Msisitizo  watolewa kwa kamati za ujenzi kuongeza uwajibikaji katika miradi ya ujenzi iliyo katika maeneo husika. Lengo likiwa ni kuhakikisha miradi inasimamiwa kuanzia mwanzo wa ujenzi wa msingi na kufuata miongozo ya ujenzi iliyotolewa na serikali. Ujenzi wa miradi hiyo unapokamilika unatakiwa  uendane na thamani ya fedha iliyowekwa.

Hayo yamejiri katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipotembelea miradi ya ujenzi inayoendelea katika shule za msingi wilayani Karatu. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea shule ya msing G-Arusha iliyopewa kiasi cha million 40 kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba viwili vya darasa. Ameelekeza kamati ya ujenzi kusimamia vyema ujenzi  na kuhakikisha fundi anaongeza nguvu kazi ili ujenzi wa vyumba hivyo vya darasa viweze kukamilika katika muda ulioainishwa kwenye mkataba wa ujenzi.

Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea shule ya msingi Karatu na kukagua ujenzi wa darasa lilojengwa na mfadhili mpaka hatua ya lenta na kuweka madirisha na milango. Katika ujenzi huo serikali imetoa kiasi cha million 12 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa darasa. Sambamba na kutembelea ujenzi wa chumba hicho cha darasa ameelekeza uongozi wa shule ya msingi Karatu kutoa taarifa ya mchanganuo wa fedha za ujenzi ulivyotumika.

Akiwa katika shule ya msingi Kainam Rhotia Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa madarasa mawili na ofisi yanayojengwa na mdau wa elimu Kamitei foundation. Madarasa hayo mawili yapo katika hatua za umaliziaji na yanatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi ujao Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa vyumba vingine viwili vya madarasa ambavyo vinafanyiwa ukarabati na wadau wa elimu Kamitei foundation. Amepongeza jitihada hizo za wadau wa elimu zinazofanywa katika shule ya Kainam rhotia ambazo zimelenga kuboresha miundo mbinu ya elimu.

 

Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea shule ya msingi Hareahbi na kujionea ujenzi wa nyumba ya walimu two in one inayojengwa na wadau wa elimu Kamitei foundation. Ujenzi huo umefika katika hatua ya lenta na unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa kumi. Mh. Kayanda ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba hizo. Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametoa kiasi cha mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa boma la darasa katika shule ya msingi Hareahbi. 

Katika ziara hiyo Mhandisi wa ujenzi, Ndg. Riziki Msite ametoa maelekezo kwa kamati za ujenzi kutoa taarifa kwa mhandisi wa wilaya wa kila hatua ya ujenzi inayofanyika. Ili Mhandisi athibitishe na kujiridhisha na aweze kutoa idhini ya  mafundi kuendelea na hatua nyingine za ujenzi. Amesema lengo ni kuhakikisha hakuna makosa yanafanyika ili ujenzi uendane vigezo vilivyotolewa na serikali. Katika ziara hiyo Mhandisi Msite ametoa maelekezo mbalimbali ambayo mafundi ujenzi wanapaswa kuyazingatia ili kutimiza vigezo vya ujenzi katika miradi.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.