Marekani imeifunga kambi ya muda iliyokuweko chini ya daraja huko Del Rio, jimboni Texas karibu na mpaka wa Mexico na kuondoa mabaki ya mwisho kwa kutumia tingatinga. 

Hivi karibuni, kulikuwa kumebakia watu 200 tu katika kambi hiyo, wengi wao wakiwa wahamiaji kutoka Haiti. 

Siku chache zilizopita bado kulikuweko maelfu ya watu karibu na Daraja la Kimataifa linaloiunganisha Del Rio na Ciudad Acuna nchini Mexico. 

Marekani iliwarejesha kwa ndege maelfu ya wahamiaji kutoka Haiti wiki hii. Na maelfu wengine walihamishiwa kwenye makazi mengine kando ya mpaka.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles