AfricaSwahili News

Kardinali Pengo Apewa Cheti Cha Heshima Akitimiza Miaka 50 Ya Upadri

 

Serikali imempatia cheti maalum Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki jimbo la Dar es  Salaam Mwanadhama Polycarp Kardinali Pengo kutambua mchango wake uliotukuka katika kanisa na jamii ya watanzania kwa miaka 50 ilitopita.

Cheti hicho kimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na kimekabidhiwa kwa Kardinali pengo na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango wakati wa maadhimisho ya misa takatifu ya miaka 50 ya upadri wa kardinali Pengo.

Katika salamu zake Rais Samia amesema serikali inathamini mchango mkubwa wa Kardinali pengo katika malezi ya kiroho hususan kwa watoto na vijana.

Amesema pia serikali inatambua jitahada za Kardinali Pengo katika kukuza na kuimarisha uhusiano mwema na dini nyingine, usuluhishi wa migogoro ambayo ilitaka kuigawa jamii na kuimariaha huduma za elimu na afya.

Rais Samia amesema kila sehemu alipofanya kazi Kardinali Pengo amedumisha amani, umoja, upendo na utengamano katika taifa na kuwa nguzo kuimarisha ushirikiano baina ya kanisa na serikali lakini pia kinara wa kukemea maovu katika jamii bila uoga.

Amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi yote ya kipaumbele aliyianzisha Rais wa awamu ya tano hayati Dk John Magufuli pamoja na miradi mingine mipya.

Pamoja na cheti Rais Samia pia ametoa fedha kuchangia ujenzi unaoendelea wa kanisa aliloanzisha Kardinali Pengo eneo la Makurunge wilaya ya Bagamoyo.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.