More
  - Advertisement -

  Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati waanza kazi rasmi

  -

  - Ad Keep reading below -

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali, leo tarehe 8 April, 2021, wameanza kazi rasmi katika Wizara ya Nishati baada ya kuapishwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushika nyadhifa hizo  April 6, 2021.

  Baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, viongozi hao walifanya mazungumzo na Menejimenti ya Wizara pamoja na  watumishi.

  - Ad Keep reading below -

  Akizungumza na Menejimenti ya Wizara pamoja na Watumishi, Katibu Mkuu  Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja amewataka kufanya kazi kwa  bidii, uaminifu na uadilifu.

  Aidha, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili Wizara iweze kufanikisha shughuli zake zote, na malengo yaliyopangwa yaweze kutekelezeka kwa urahisi.

  - Ad Keep reading below -

  Vilevile, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo, kuwa wabunifu ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao, na pia kuwawezesha watumishi waliopo chini yao ili wafanye majukumu yao kwa ufanisi.

  ALSO READ  Houthis delay UN inspection of damaged oil tanker off Yemen

  Pia amewataka Wakuu hao wa Idara na Vitengo, kuweka usawa katika mgawanyo wa majukumu ili kila mtumishi aweze kuwatumikia watanzania kwa nafasi aliyonayo.

  Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, wa Wizara ya Nishati, Kheri Abdul Mahimbali, amewataka watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi kutumia uzoefu wake katika sekta ya Nishati ili kufanikisha majukumu ya Wizara.

  ALSO READ  Hijab crisis: Kwara is Muslim State, take your missionary schools to Rivers – Islamic group warns

   

  - Ad Keep reading below -

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Ministry Plans Monthly Cash for Jobless Kenyans in 5 Counties

  The Ministry of Labour has offered hope for Kenyans who were rendered jobless as a result of the government's directive to lock down 5 counties...

  Twitter Unveils Algorithmic Fairness Initiative to Offer More Transparency in Its AI

  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -