Msaanii A list kutoka Bongo, Ommy Dimpozi, ameweka wazi kwa namna Mfalme wa Bongo fleva Ali Kiba, alivyopambana kuhakikisha anapona wakati anapitia changamoto za kiafya hata akimkuta anamsaliti na mkewe yeye atamsamehe tu.

Ommy ameyasema hayo jana katika hali ya utani kwenye uzinduzi wa Album ya Ali Kiba iliyopewa jina la ‘Only One King’.

Dimpozi akielezea namna Ali alivyopigania hali yake ya ki-afya, amesema Kiba alimuonea huruma wakati wa maandalizi ya harusi (ya Ali Kiba) ambapo alimshuhudia akipata tabu wakati wakiwa wanakula chakula.

Dimpozi anakiri kuwa King Kiba ndiye aliyemuomba Rafiki yake wa karibu sana Gavana wa Mombasa, Hassan Ali Joho, kumsaidia yeye kutokana na kujuana na Madaktari wazuri nchini Kenya na baadae wakakubaliana kwenda kuanza matibabu Jijini Nairobi.

Watu hawajui, lakini Ali alipambana sana mpaka Mwenyezi Mungu kunipa nafasi nyingine ya kuishi. Mimi hata nikimfumania Ali na mke wangu ninamsamehe kabisa. Natania tu,” Dimpozi.

Tagged in:

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles