AfricaSwahili News

Kigogo wa juu wa jeshi Nigeria ashambuliwa na kuuawa kwa risasi na watu wasiojulikana

Watu wasiojulikana nchini Nigeria wamempiga risasi na kumuua mmoja wa vigogo wa jeshi la nchi hiyo, Meja Jenerali Hassan Ahmed.

Meja Jenerali Ahmed aliuawa usiku wa alhamisi nje kidogo ya Abuja wakati gari lake liliposhambuliwa kwa risasi, akitokea jijini Lokoja kwenda Abuja, akiwa na familia yake.

Dereva aliyekuwa anaendesha alijeruhiwa na mwanake mmoja aliyekuwewepo kwenye gari hiyo anayetajwa kuwa dada wa meja huyo, Safina Ahmed alitekwa.

Jeshi la nchi hiyo limeyaelezea mauaji hayo ni ‘tukio la kusikitisha’, huku kuuawa kwake kukingeza hofu ya usalama nchini humo.

Meja Jenerali Ahmed hivi karibuni aliteuliwa na mkuu wa majeshi ya nchi hiyo kuwa Mkurugenzi wa jeshi makao makuu. Haijajulikana mara moja kina nani hasa walio nyuma ya shambulio hilo na lina lengo gani hasa.

Kwa muda sasa nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio ya kiusalama ambapo makundi mbali mbali yenye silaha yamekuwa yakiendesha mauaji na utekaji wakilengwa raia na wanajeshi. Kutokana na vitendo hivyo Mamlaka nchini humo zimekuwa zikitupiwa lawama kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.