Kijana anayeendesha bodaboda Liberia amekuwa shujaa wa kitaifa baada ya kuokota dola 50,000 ambazo zilikuwa zimepotea za mwanamke mmoja ambaye ni mfanyabiashara maarufu kaskazini mashariki mwa mpaka wa Ivory Coast.

Kijana huyo mdogo, Emmanuel Tolue, alizikuta pesa zikiwa kwenye mfuko wa plastiki barabarani na alisikia tangazo kwenye radio ambapo mwenye fedha Musu Yancy,aliomba sana atakayeziona amsaidie kwa kumrudishia..

Kijana huyo alimjulisha kuwa amezipata katika ofisi za serikali ya mitaa.

Bi Yancy ameiambia BBC kuwa amemzawadia dola 1,500 (£1,100) pamoja na zawadi nyingine.

Mwanamke huyo alifurahi sana kupata taarifa ya kuwa anazipata pesa zake, alipiga kelele kumsifu Mungu mpaka sauti ilikuwa inakaribia kupotea.

Watu wengi walimsifia kijana huyo kwa kufanya usamaria mwema wa aina hiyo.

Jambo kama hilo la ambalo kijana wa bodaboda amelifanya si jambo la kawaida kutokea Liberia, mara baada ya vita.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles