More
  - Advertisement -

  Kim Kardashian ajiunga klabu ya mabilionea

  -

  - Ad Keep reading below -

  Nyota wa Marekani wa kipindi cha TV Kim Kardashian West ameingia katika klabu ya matajiri wakubwa.

  Utajiri wake umefikia thamani ya dola bilioni moja(£720m) unaotokana na vipodozi, mavazi pamoja na mapato yake ya kipindi cha TV, mikataba mbalimbali na uwekezaji, Jarida la Forbes limeandika.

  - Ad Keep reading below -

  Kwa sasa Kim Kardashian ni miongoni mwa idadi ya watu 2,755 ambao wameainishwa katika orodha ya mabilionea duniani iliyowekwa na jarida la Forbes.

  Muasisi wa Amazon Jeff Bezos anaongoza kwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 177.

  - Ad Keep reading below -

  Wamarekani wengine ambao waliongezwa kwa mwaka uliopita ni muasisi wa programu ya mahusiano ya Bumble dating app,Whitney Wolfe Herd ($1.3bn), mtengeneza filamu Tyler Perry ($1bn) na Miriam Adelson ($38.2bn).

  ALSO READ  Manchester City yaongeza muda wa ushirikiano na QNET

  Kim Kardashian West na mume wake ambaye Kanye West alikuwa tayari kwenye orodha kwa kuwa na dola bilioni 1.8 lakini dada yake wa kambo Kylie Jenner aliondolewa katika orodha hiyo mwezi Mei mwaka jana. Jarida hilo lilimshutumu kwa kudanganya thamani ya biashara ya vipodozi.

  ALSO READ  Wazazi wa watoto shule ya St Jude waeleza sababu ya kuandamana

  Jarida la Forbes limejumuisha thamani ya dola milioni 780 iliyoongezeka na kufikia dola bilioni moja inayotokana na biashara yake ya vipodozi na kampuni ya mavazi.

  Kampuni ya vipodozi ya KKW Beauty ilianzishwa mwaka 2017 na kampuni ya nguo ya Skims ilianzishwa miaka miwili iliyopita baada ya kuzindua vazi aliloliita Kimono, ingawa ilishuka kutokana na shutuma za kitamaduni.

  - Ad Keep reading below -

  Bi.Kardashian West aliuza 20% ya kampuni ya vipodozi ya KKW Beauty mwaka jana kwa dola milioni 200, katika mkataba wa biashara ambao unafika thamani ya $1bn.

  Mradi wake wa sasa wa Skims una nguo za ndani na nguo ndefu na umesaidia katika mafanikio yake.

  ALSO READ  Sudan: 'US is not a charity', nothing is for free

  Nyota huyo ametumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zake , sasa akiwa na wafuasi milioni 213 kwenye Instagram; wafuasi milioni 69.7kwenye Twitter.

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Oduduwa Republic: Tell us your plans for Yoruba Muslims – Islamic group tells agitators

  The Ooni of Ife, Adeyeye Enitan Ogunwusi Ojaja II, has appealed to Nigeria’s Ambassador Designate to Jamaica, Belize, Haiti and Dominican Republic, Dr. Maureen...

  AUDIO | Christina Shusho – Wanawake Tunaweza | Download

  Download | Christina Shusho – Wanawake Tunaweza https://dl.soundbykiki.com/uploads/Christina%20Shusho%20-%20Wanawake%20Tunaweza.mp3  ...

  India Records More Than 200,000 New COVID Cases Thursday | Muhabarishaji News Agency

  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -