By Hadija Jumanne

By Fortune Francis

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Jumatatu Januari 10, 2022 imekubali pingamizi la kutopokea sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama moja ya kielelezo lililowekwa na upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

SOMA:Kesi ya kina Mbowe kuanza kesho kwa uamuzi

Katika pingamizi hilo upande wa utetezi uliiomba Mahakama isipokee kielelezo hicho kwa kuwa hakikufuata utaratibu wa ukamataji wa mali wakati upande wa mashtaka ukiiomba mahakama hiyo izipokee sare hizo zinazodaiwa kukutwa na mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi, Halfani Bwire Hassan, ziwe kielelezo cha ushahidi wake.

Uamuzi huo umetolewa na leo Jumatatu Januari 10, 2022 na Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo.

Hapa ni sehemu ya uamuzi uliotolewa na Jaji Joachim Tiganga katika pingamizi hilo….

Advertisement

Jaji Joachim Tiganga ameshaingia mahakamani kwa ajili ya kusoma uamuzi

Mawakili wa pande zote wameanza kujitambulisha.

Jaji Tiganga anawaita majina washtakiwa mmoja baada ya mwingine

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri linakuja kwa ajili ya kupokea uamuzi na kuendelea na ushahidi

Jaji: Upande wa utetezi?

Kibataka: Mheshimiwa Jaji nasisi tupo tayari kupokea uamuzi na kuendelea na kesi

Jaji: Nilitoa maelekezo hapa mahakamani, mtu yoyote anayeingia amwe amevaa maski (barakoa) kwanini wengine hawajavaa??

Jaji: Nina excuse ya wakili mmoja ambaye havai …sasa wengine je?

Wakili Mallya: Mimi nina tatizo kidogo lakini nimechukua tahadhari zote za kujikinga na Uviko-19.

Baada ya Maelezo hayo, mmoja wa wafuasi wa Chadema alitoka nje na kwenda kuvaa barakoa kisha kuingia ndani huku watu wengine waliokuwepo ndani ya mahakama waliokuwa wameshusha barakoa zao chini ya pua,  wakizipandisha barakoa zao juu ya pua

Jaji Tiganga ameanza kusoma uamuzi wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Jaji Tiganga: Upande wa utetezi wao walianza na hoja moja kuwa kielelezo hicho namba 14 (Hati ya ukamataji mali) kilichezewa hivyo wanaomba ihesabike kuwa kisipokelewe na mahakama kwa sababu hajikidhi vigezo.

Jaji Tiganga: Kwa upande wa mashtaka wao walijibu hoja za upande wa utetezi kwa kueleza kuwa upande wa utetezi wametafsiri vibaya tafsiri ya sheria na kusema suala la utunzaji wa vielelezo linafahamika  na upande wa mashtaka haulazimishwi kutoa vielelezo vyote.

Jaji Tiganga: Upande wa mashtaka wakaendelea kuomba korti ipokee kielelezo hicho kwa sababu kimekidhi vigezo.

Jaji: Upande wa mashtaka uliendelea kueleza kuwa shahidi wa nane wa upande wa mashtaka SP Jumanne Malangahe aliandika maelezo namna alivyomtambua shahidi na namna alivyowasilisha vielelezo hivyo kwa mtunza vielelezo aitwaye Sajenti Johnstone.

Hivyo upande wa mashtaka waliomba mahakama ipokee kielelezo hicho kwa sababu hakikuchezewa na kilifuata mnyororo wa utunzaji.

Upande wa mashtaka waliendelea kuiomba mahakama ipokee kielelezo hicho baada ya kupitia mnyororo wa utunzaji wa kielelezo.

 Jaji: Pia upande wa mashtaka walieleza kuwa shahidi wa nane SP Jumanne Malangahe ndio aliyevikamata vielelezo hivyo na ndio yeye aliyevitoa mahakamani baada ya kuvitoa kwa mtunza vielelezo.

Jaji: Upande wa utetezi wakiwasilisha nyongeza yao ya kuwapinga vielelezo hivyo walieleza kuwa shahidi alitakiwa aviandike vielelezo hivyo katika notebook yake ili kuepuka vielelezo visichezewa.

Jaji: Hoja kuhusu Competent iliyotolewa na upande wa utetezi kuhusu kielelezo hicho kwamba hakukuwa na uthibitisho uliotolewa kama kweli sare hizo ninmali ya JWTZ

Jaji- Wakili Mallya alidai kuwa vielelezo hivyo ni vya kijeshi na nilitakiwa kutolewa kwa majina ya kijeshi.

Mallya alidai mfano kuna kielelezo shahidi alikita kuwa ni koti la mvua au ponjoo wakati kwa lugha ya kijeshi linatambulika kama sleeping bag.

Jaji: Wakili Mallya aliendelea kueleza kuwa kwa mazingira hayo shahidi huyo SP Jumanne Malangahe hana uelewa wa kutosha kuhusiana na vielelezo vyenyewe, hivyo wanaomba vielelezo hivyo visipokelewe.

Mallya aliendelea kueleza kuwa shahidi wa nane huyo hajaithibitishia wala hakuleta ushahidi wake mahakakani kama ni mtaalamu wa utambuzi wa vifaa vya kijeshi

Jaji: Kwa upande wa mashtaka kupitia wakili Kidando akijibu hoja ya wakili Mallya alidai kuwa shahidi alitambua vielelezo hivyo kwa alama alizoweka mwenyewe na kwamba sio lazima shahidi kuwa mtambuzi bali anatakiwa kuwa na ufahamu wa vifaa vya kijeshi.

Jaji: Hivyo upande wa mashtaka walidai maelezo aliyotoa Mallya kuwa vielelezo hivyo vimetolewa kwa majina tofauti havina mashiko kwa sababu Mallya yeye sio shahidi katika kesi hii, hivyo wanaomba Mahakama ipokee kielelezo hicho kwa sababu shahidi alitambua vielelezo hivyo kupitia alama alizoweka wakati wa ukamataji.

Jaji: kourti baada ya kupitia hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa na Mallya, inatupilia mbali pingamizi hili.

Jaji: Kifungu pia cha 22(3) d  cha Sheria ya Uhujumu Uchumi inasema pia kuwa ni lazima kutoa risiti but pia PGO ya 226 (2,5) na yenyewe inasema kuhusiana na utolewaji wa risiti

Na mwisho Guidelines ya Mahakama Chapter 05 Paragraph ya 5 (f) inasema kuwa inatakiwa kutolewa risiti ya mali zilizokuwa zinakamatwa

Hakuna sehemu inayosema kuwa pale mahala ambapo risiti haijatolewa basi seizure Certificate itumie kama mbadala wa risiti

Kwa upande wa utetezi walikataa mwaliko huo kwa kuomba mahakama ikatae mwaliko huo kwamba risiti na seizure Certificate ni nyaraka mbili tofauti

Katika eneo hilo Mahakama inamaoni kuwa swala la risiti Mahakama imewekwa wazi na ni muhimu itumike

Suala la Certificate of Seizure (hati ya ukamataji) kutumika badala ya Risiti kuna Maamuzi ya mahakama ya Rufani ya ANDREA AGUSTINO na wenzake ikiwa imeamliwa huko Tanga katika Rufani ya Jinai.

Mahakama ilipo itwa Kuona Kuwa Risiti Itumike Mbadala wa Certificate of Seizure ilisema Kuwa

Basi ni wazi kuwa Mahakamani ya Rufani ilishaona kuwa jambo hili no vitu viwili tofauti na Mahakama inaona kuwa kutokutolewa kwa risiti Ni mambo mawili tofauti.

Baada ya kuwa tumeona kutokutolewa kwa risiti kuna athari, Mahakama ya Rufani Iliyoketi Iringa na Ilikuwa aime Quote with Approval katika Kesi ya PATRICK JEREMIAH Vs JAMHURI 34 / 2016

Kwa sababu hiyo Mahakama hii Inaona Kuwa Kushindwa Kutoa Kwa risiti ni Fatal na Jambo hili lina athiri Admissibility.

Kutokana na malekezo hayo ya Kisheria yakiyoelezwa katika PGO hiyo ni wazi kuwa alama iliyiwekwa siyo alama ambayo PGO 229 imeitambua na kuelekeza

Hata kama alama hiyo ingekuwa imevumiliwa basi kama ingekuwa alama hiyo iliwekwa mbele ya mashahidi hao basi ingevumilia

Hivyo, katika utaratibu huo Mahakama ina maoni kwamba alama hiyo iliyowekwa imekiuka PGO 229 kwa maana hiyo inaathiri afya ya kielelezo hicho na kuathiri Competence

Na nikitafuta matakwa ya Adminsibility kuwa Polisi ofisa alitakiwa kutoa risiti ya ku -acknowledge kukamata vielelezo hivyo

Hata hivyo jatika koja hiyo upande wa utetezi wanasema kuwa mtu yoyote ambaye anafanya upekuzi lazima atoe risiti baada ya upekuzi kama ambavyo Sheria inalekeza

Wanasema kuwa shahidi wa nane wa upande wa mashtaak hajasema kuwa ametoa risiti wala hajatoa nakala yoyote mahakamani kama alitoa risiti

Kwa namna hiyo wakialika sheria kwa kutokutoa risiti.

Katika majibu yake Wakili Kidando anasema kwa kufanya upekuzi na kukamata mali, Shahidi namba nane alitoa hati ya ukamataji mali ( Seizure Certificate).

Pia upende wa mashtaka wakasema kuwa kwa kutolewa Seizure Certificate ambayo ina content sawa na risiti wakaomba Mahakama wa one kuwa Seizure Certificate ionekane kama risiti

 Upande huo wa mashtaka waliendelea kwa kuomba Mahakama Izingatie Sehemu ya Pili katika sehemu A ya CPA, 2 (a) D Mahakama Ione kuwa Kuwepo Kwa Seizure Certificate ni sawa na Kutolewa Risiti

Hivyo, nakubaliana na upande wa utetezi kama ambavyo wameieleza Mahakama kuwa panapokuwa umefanyika upekuzi katika nyumba, box au eneo ofisa ambaye amekamatwa mali anatakiwa kutoa risiti juu ya mali alizokamata na nukuu Kifungu cha 38 (3)  ya CPA

Kifungu Kingine kinachohusika kutolewa na risiti ni kifungu cha 35(3) ya Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322

Uamuzi wa Jaji Tiganga: Katika hali ya kawaida Mahakama ilitakiwa kuishia hapa, lakini kuna mwaliko wa Kibatala kuwa Mahakama izingatie kuwa unatafuta nini kila inapokuwa Sheria inakiukwa lakini wanapewa nafasi upande wa mashtaka

Nimeona hakuna cha ku reconcile katika maamuzi ambayo nimeshayatoa, maamuzi yote niliyo yatoa ni maamuzi halali hivyo Mahakama inaona hoja hiyo halikuwa na mashiko na naitupilia mbali

Mahakama inaona hoja zote zilizoletwa na upande wa utetezi hayakuwa na mashiko isipokuwa mapingamizi mawili ya Lebelling na kutokutoa risiti

Na kwa mapingamizi haya Mahakama inaona yana merit na sababu nilizotoa mahakamani nakataaa vielelezo hivyo na ninatoa amri.

Jaji Tiganga baada ya kutoa uamuzi huo, Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia.

Jaji: Haya upande wa mashtaka tuanendela na ushahidi.

Baada ya Jaji kutoa uwamuzi shahidi wa nane anaendelea na ushahidi.

Jaji: Shahidi tunakukumbusha uko chini ya kiapo na utaendelea kutoa ushahidi wako.

Wakili Kidando anamuongoza Shahidi kuendelea na ushahidi.

Shahidi Jumanne Malangai Tarehe 24/2020 nikiwa Arusha nilifika eneo moja nililoliona kwenye mchoro linaitwa kilombero na kubaini ni soko lililoko katikati ya Jiji upande wa magharibi limepakana na gereza la kisongo, kutokea hapo umbali mfupi upande wa kulia kuna hilo soko la kilombero.

Nilipo endelea na upelelezi kesho yake tarehe 25, alikamatwa mtuhumiwa Elia Kaaya ambaye baadae aliachiwa baada ya upelelezi kukamailika

Justin Kaaya aliachiwa baada ya ushahidi kuonyesha alikuwa hausiki

Tuliendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine ambapo tarehe 10/9 alikamatwa mtuhumiwa mwingine ambapo naebaliachiwa baadaa ya upelelezi kukamillika.

Mshtakiwa huyu kwa taarifa tulizopata alikuwa Miongoni mwa watuhumiwa waliokuwa washiriki kufanya uhalifu.

Tulifika mkoani Tabora na kukamata mtuhumiwa mwingine Gabriel Mhina tarehe 19/9/2020 nae alikuwa ni askari wa JWTZ Kikosi cha 92 KJ nae aliachiwa baada ya ushahidi kutokamilika

Kuna mtuhumiwa mwingine tulimkamata Mwanza tarehe 19 wakati tukiwa tunamfuatilia mtuhumiwa mwingine Malima ambaye nae aliwahi kuwa JWATZ Kikosi cha 92 KJ

Asubuhi nlitembelea eneo lingine Mwanza mjini ambapo kuna mkutano ya barabara kuelekea mabatini upande wa kushoto kuelekea benki ya BOT kuna kituo cha mafuta kinachoitwa Puma Energy

Tulimkamata Malima eneo la mjini linaloitwa pasians na baadae aliachiwa baada ya kuhojiwa na kuonekana hakuna ushahidi wa kumpeleka mahakamani

Baada ya hapo upelelezi uliendelea na tarehe 22/11 aliketwa mtuhumiwa wa nne Freeman Mbowe ili niweze kumuhoji

Baada ya mtuhumiwa kuletwa mbele yangu na kujitambulisha nilimuonya kuhusiana na tuhuma za kula njama za kutenda ugaidi na baada ya kumuonya alikubali kuandika maelezo yake mbele ya Wakili wake alimtambulisha Fred Khiwelo.

Wakili Kibatala: Haya yote anayoeleza shahidi yako kwenye rekodi sioni kama yana tija

Shahidi: Baada ya kumuhoji Mbowe alisema hawezi kutoa maelezo hadi pale atakapofika mahakamani.

Jina la Alfani Bwire nililiandika kutokana na matamshi yake mwenyewe

Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.

Wakili Kibatala:  Kutokana na yale mazoea yetu tuliyojiwekea kupumzika saa saba ningeshauri tupumzike dakika 45 ili tukirudi tuweze kuendelea

Wakili Kidando: Mheshimiwa hatuna pingamizi

Jaji. Tunabreak kwa dakika 45 tutarudi hapa saa saba na nusu.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles