Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano amesema juhudi za kushirikisha kikundi kilichojitenga cha upinzani cha Renamo zinapaswa kuendelea baada ya kiongozi wake kuuawa Jumatatu.

Jenerali Mariano Nhongo aliuawa na vi vikosi vya usalama katika mkoa wa Sofala ya kati.

“Sikutaka kifo cha mtu yeyote lakini watu lazima walindwe. Na watu wakilindwa , huenda kukazuka makabiliano na maadui,” alisema Bwana Chissano, aliongeza kumekuwa na nafasi ya mazungumzo na kiongozi wa waasi.

Jenerali Nhongo alipinga mmkataba wa amani ambao Renamo ilifikia na serikali mnamo 2019 na alikuwa akifanya mashambulio dhidi ya raia na vikosi vya usalama.

Karibu nusu ya wapiganaji wake watiifu 5,000 lwalikuwa wameunga mkono mkataba huo.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles