in

Kocha wa Yanga afunguka kuhusu Ubingwa wa Vpl

Kocha wa Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu 2020/21 Young Africans, Juma Mwambusi amesema kuwa kikosi chake kitacheza mchezo wa kushambulia mwanzo mwisho dhidi ya Biashara United hapo kesho huku akiongeza kuwa wao bado hawawezi kusema wamekata tamaa na Ubingwa kwakuwa wapo kwenye mapambano.

Mwambusi ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari ”Kikubwa ni kumshuru Mungu tumeamka salama, tulicheza tukapata pointi moja na KMC, matokeo yale tumeshasahau, tumekwenda kufanya marekebisho mawili, matatu ambayo yalitokea kwenye mechi iliyopita, hii mechi yetu itakuwa na mabadiliko kwasababu tumeshaona nini ambacho tulikuwa tunafeli na kwa nini tulikuwa hatuwezi kuzitumia nafasi ambazo tulizokuwa tunazipata.”

”Tumelifanyia kazi na wachezaji wameelewa na wapo tayari kwa kucheza, kikubwa tunaheshimu timu zote zinazoshiriki ligi kuu pamoja na Biashara United, ni timu ambayo unaona kwenye nafasi ya ligi bado ipo juu na sisi sasa tunacheza kwenye uwanja wa nyumbani. Kimikakati tumekwenda sawa sawa, bado nasema mpira wetu sisi utakuwa sio wa kurudi nyuma, utakuwa ni wakushambulia, tunaanza kushambulia mpaka dakika ya mwisho, kikubwa zaidi ni kwamba tumejiandaa na tupo tayari kwa mpambano.”- Kocha Mwambusi

Akizungumzia kuhusu Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu huu Kocha Mwambusi amesema ”Yanga bado tupo kwenye mapambano, haijalishi matokeo tuliyopata nyuma, lakini hatuwezi kusema tunakata tamaa, tupo kwenye mapambano na bado mechi zimebaki kama 10 kwa hiyo tunaangalia kwenye mechi hizi tutakachokivuna, juhudi yetu kubwa ni kuhakikisha tunavuna pointi tatu kwa kila mchezo.”

Hapo kesho Yanga watashuka uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku kuwakabili Biashara United ambao wapo kwenye nafasi ya nne huku Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya sare 1 – 1, katika mechi iliyopita dhidi ya KMC FC.

60% uranium enrichment obtained by Iranian scientists

Banditry: Gov Matawalle suspends Zamfara District Head