AfricaSwahili News

Kuna shule wanafunzi hawajawahi kumuona mwalimu wa hesabu, fizikia – Waziri Ummy Mwalimu

 

Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema bado kuna upungufu wa walimu wa somo la sayansi katika shule za sekondari nchini Tanzania.

Amesema kwa uchambuzi uliofanywa  unaonyesha kuna shule takribani 1000 za sekondari ambazo wanafunzi wake hajawahi kukutana uso kwa uso na mwalimu wa somo la Fizikia na kwamba shule takribani 400, wanafunzi hawajawahi kumuona mwalimu wa hesabu akiingia darasani.

Ummy ameyasema hayo leo Alhamisi Juni 10,  2020 alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum (CCM), Hawa Mchafu kuhusu lini  walimu wa sayansi watapelekwa katika Mkoa wa Pwani.

“Tunakiri kuwa na uhaba wa walimu wa sayansi. Kwa uchambuzi uliofanywa ndani ya miezi mitatu unaonyesha takribani shule 1000 za sekondari ambazo wanafunzi wake hajawahi kukutana uso kwa uso na mwalimu wa somo la Fizikia. Shule zipatazo 400 ambazo hazijawahi kuona mwalimu wa hesabu akiingia darasani,” amesema Ummy.

Amebainisha kuwa ipo fursa ya kutumia (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)  ili kuwawezesha kusoma kupitia mtandao.

“Hili tumeliona ipo fursa ya kutumia maendeleo ya ICT ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kupitia mtandao…, tutaajiri walimu wazuri na kurekodi mada zote kuwawezesha kusoma kwa njia ya mtandao,” amesema Ummy.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.