AfricaSwahili News

Kura ya imani nchini Israel yakaribia

Ofisi ya spika wa bunge la Israel imesema itawaarifu rasmi wabunge siku Jumatatu kuhusu tangazo la upinzani la muungano wa kumvua mamlaka waziri mkuu mkongwe wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa tamko hilo litaanzisha maandalizi ya kura ya imani katika serikali hiyo mpya ambayo sasa itapigwa siku ya Jumatano ama Jumatatu itakayofuata. 

Tangazo hilo la jana jioni lililotolewa na mwenyewe Spika Yariv Levin, mshirika wa karibu wa Netanyahu, linaondoa hofu kuwa chama chao cha Likud kinachoegemea siasa za mrengo wa kulia kingeweza kupata njia za kuzuia uundaji wa muungano huo ambao unahitimisha miaka 12 ya utawala ya Netanyahu. 

Kimsingi, muungano huo uliotangazwa na kiongozi wa upinzani, Yair Lapid, dakika chache kabla ya muda wa mwisho usiku wa Jumatano, unapaswa kuwa na wingi mdogo wa kura katika kura hiyo ya imani.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button