Kufuatia kurudi kwa meli ya Mv Victoria Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kagera wamesema walipiti kipindi kigumu cha kusafirisha bidhaa kutoka mkoani humo kwenda mkoa wa Mwanza kutokana na meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU kusitisha safari zake kwaajiri ya kufanyiwa matengenezo.

Akizungumza na Fullshangwe Blog Bwana Amri Athuman mfanya biashara wa ndizi, palachichi pamoja na mazao mbalimbali kutoka Bukoba kwenda Mwanza alisema kurudi kwa Mv Victoria itawasaidi sana kuepukana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kipindi meli hiyo ipo kwenye matengenezo.

 “ Kukosekana kwa meli hii imepelekea sisi kama wafanyabiashara kutumia gharama kubwa kusafirisha bidhaa zetu kutoka Kagera kwenda Mwanza kwani tumekuwa tukitumia usafiri wa maroli ambavyo ukiangalia gharama zake nikubwa ukilinganisha na gharama za meli katika sualazima la usafirishaji”.

Nae  mkuu wa mkoa wa kagera  Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa safari za meli hiyo inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza itarejea rasmi Octor 15 mwaka huu.

Kauli ameitoa jana akiwa ofisini wakati aluipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka wananchi sasa kuwa tayali kwa mapokezi mazuri ya meli hiyo.

“Meli ya NEW MV VICTORIA hapa kazi tu iliyositisha safari zake kwaajiri ya kufanyiwa matengenezo inatarajia kurejea Octoba 15 mwaka huu  na itaanza safari zake kama kawaida”. Amesema Mbuge.

Hata hivyo ameongoza na kusema kuwa Ikumbukwe kuwa, meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU ilisitisha safari zake mnamo tarehe 27 septemba mwaka huu.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles