Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limeingia makubalino ya mkataba wa miaka mitatu na Benki ya NBC kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara na msimu huu.

Rais Wallace Karia

Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Wallace Karia amesema wameingia makubaliano na NBC baada ya mchakato wa muda mrefu ambao ulikuwa na lengo la kuwekeza vizuri katika mchezo wa mpira wa miguu na kwamba Benki hiyo itatoa kitita cha Bilioni 2.5 kabla ya VAT.

Akizungumza baada ya kuingia makubaliano hayo , Rais Karia amesema kuanzia sasa Ligi Kuu itatambulika kama NBC Tanzania Premier League.

Karia amesema wamepata udhamini kutokana na Shirikisho kuaminiwa na taasisi mbalimbali kutokana na kuwa na Utawala bora pamoja na uadilifu katika rasilimali fedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NBC, Teodas Sabi amesema, udhamini huo wa Sh2.5 bilioni kabla ya VAT itakuwa ni kwa ajili ya msimu huu mpya.

Mazungumzo yalikuwa ya muda mrefu sana, tumeridhika kabisa kuingia makubaliano na TFF tunatambua mpira wa miguu ndio mchezo pekee unaopendwa zaidi Duniani,” Teodas Sabi amesema.

BY: Fatuma Muna

Tagged in:

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles