AfricaSwahili News

Ludewa: Wananchi waficha maiti na kujizuia kulia kukwepa gharama za mochwari

Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Wananchi wa kijiji na kata ya Lupanga,wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.Wamesema wamekuwa wakilazimika kuficha maiti,kuzuia matangazo na kujizuia kulia unapotokea msiba jioni au mchana majumbani mwao ili kuepuka ada ya kulaza maiti mochwari inayofika zaidi ya elfu 50,000 

Wananchi wa kijiji hicho wameeleza changamoto hiyo katika mkutano wao na mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga alipofika katika kijiji hicho ikiwa ni ziara yake anayoedelea kila kijiji ili kupata changamoto na kuzifanyia kazi huku akitoa mrejesho kwa wananchi juu utekelezaji wa baadhi ya changamoto zao za awali mara baada ya kuzifikisha katika halamashauri na vikao vya bunge

Zebedayo Mgaya ni mmoja wa wakazi wa kijiji hicho aliyeeleza changamoto hiyo huku akibainisha kuwa amewahi kufiwa hivi karibuni na ndugu yake na kulazimika kukaa kimya na maiti nyumbani kwake akihofia kutangaza kwa kuwa uongozi wa kijiji hicho ungemtaka kufikisha mwili wa marehemu mochwari iliyopo umbali wa zaidi ya KM 10 kutoka kwenye kijiji hicho huku ghalama za usafirishaji pekee zikiwa ni shilingi elfu 40 mpaka 50

“Ghalama za kusafirisha mwili kutoka hapa mpaka mochwari iliyopo Mlangali ni zaidi ya KM 10 na ghalama zake ni elfu 50 mpaka 50 na sijui kwanini ghalama ya kusafirisha maiti ni kubwa kuliko kusafirisha mahindi.Nashauri kama Mochwari ni mradi mzuri kwa wizara ya afya au halmashauri basi wajenge kila kijiji mahali ambapo mtu anaweza kufikisha maiti na kurudisha nyumbani”alisema Zebedayo Mgaya

Aidha wananchi wa kijiji hicho wamesema wamekuwa na hofu wanapopata msiba na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji kwa kuwa imekuwa ikiwalazimu kufikisha maiti katika mochwari kutokana na kuto ruhusiwa kulala na maiti huku wengi wao wakiwa hawana ada ya mochwari kwa wakati huo.

“Tumekuwa na hofu kubwa mtu akifa jioni,watu huwa hawatoi yowe na inapofika siku ya pili tunatoa taarifa ili ionekane mtu amekufa siku leo kumbe amekufa jana ili tu kukwepa ghalama ya mochwari”alieleza mwananchi mwingine mbele ya mbunge Kamonga

Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Baraka Mfaume aliyeongozana na mbunge katika mkutano huo amesema Chama kimepokea changamoto hiyo na kuelekeza ofisi ya mkuu wa wilaya kuifanyia kazi.

“Kwa desturi zetu tunawaheshimu sana ndugu zetu waliotangulia mbele za haki,uongozi wetu wa afya wamekuwa wakitutaarifu ndugu zetu wamefariki kwa tatizo gani ili taratibu za mazishi zifanyike kwa tahadhari lakini kama jambo hili halipo hivyo hapa tunaliacha kwa mkuu wa wilaya Lifanyiwe ufuatiliaji”alisema Baraka Mfaume

Naye mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga amesikitishwa na kitendo cha wananchi hao kukabiliwa na changamoto hiyo huku akitaka viongozi wa kijiji pamoja na afisa tarafa kuifuatilia changamoto hiyo na kutoa wito kwa viongozi kutoa elimu kwa wananchi ili kutoana ni kero kwao wanapopatwa na matatizo ya misiba.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.