Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Mahakama ya Juu ya Jordan yathibitisha hukumu kwa watuhumiwa wa njama dhidi ya ufalme

Advertisement Scroll To Keep Reading

Mahakama nchini Jordan imethibitisha hukumu iliyowatia hatiani maafisa wawili wa ngazi za juu kwa uchochezi na njama dhidi ya utawala wa Mfalme Abdullah wa Pili, ambazo zinamuhusisha ndugu wa kiume wa mfalme huyo. 

 
Shirika la habari la serikali, Petra, limeripoti kwamba Mahakama ya Juu iliamuwa hapo jana kwamba watuhumiwa hao walitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
 Bassem Awadallah, ambaye ana uraia wa Marekani na aliwahi kuwa mpambe mku wa mfalme, na Sharif Hassan bin Zaid, ambaye ni sehemu ya aila ya kifalme, walihukumiwa kifungo cha miaka 15 mwezi Julai na mahakama ya kijeshi. 
 
Wawili hao, walituhumiwa kupanga njama pamoja na Hamza, mrithi wa zamani wa kiti cha ufalme, na kusaka msaada wa kigeni. 
 
Mwanamfalme Hamza, ambaye aliwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani, amekanusha kuwa sehemu ya njama zozote, akisema kuwa anaandamwa kwa sababu ya kukemea ufisadi.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.