AfricaSwahili News

Majaji sita waliokataliwa na rais Uhuru Kenyatta lazima wateuliwe-Jaji mkuu wa Kenya

Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza wito wake kuwa majaji sita walioachwa kwenye orodha ya wale walioteuliwana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni lazima wateuliwe .

Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa Daniel Musinga kama rais wa Mahakama ya Rufaa, alisema wakati huo ulikuwa mchungu, kwa sababu majaji wanne – ambao waliteuliwa kwa korti ya Rufaa – walikuwa bado hawajateuliwa.

Koome alisema Mahakama iko katika hatari ya kutekwa na idara na vile vile “watu ambao sitawataja”.

Koome pia alielezea wasiwasi wake kuhusu ufadhili mdogo wa Mahakama na akamuambia Spika wa Bunge la taifa Justin Muturi moja kwa moja, akisema kwamba mgao wa Sh37 bilioni ulikuwa mdogo sana kati ya Bajeti ya Sh3.6 trilioni iliyosomwa siku Alhamisi.

Koome alisema Idara ya Mahakama ilikuwa ikifanya kazi katika “jumba la makavazi” ambalo lilikuwa katika hali mbaya na akashangaa kwa nini wizara ya Afya haijalitaja jengo hilo kama hatari ya kiafya lisilofaa kutumiwa

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button