AfricaSwahili News

Makombora matatu ya roketi yalenga Ikulu ya Afghanistan

Takriban mashambulizi matatu ya roketi yamelenga eneo karibu na Ikulu ya Rais muda mfupi kabla ya Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani kutoa hotuba yake ya kuadhimisha sikukuu ya Eid al-Adha.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan Mirwais Stanikzai amesema hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo ya roketi yaliyopiga nje ya Ikulu.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo ingawa polisi walifika haraka katika eneo la tukio na kushika doria.

Raia wa Afghanistan wana wasiwasi juu ya usalama wa nchi hiyo baada ya vikosi vya usalama vya kimataifa kuondoka nchini humo katika wakati ambapo kundi la Taliban linaendelea kuchukua udhibiti wa wilaya kadhaa.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.