Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Makubaliano ya kero za Muungano kuanikwa Jumapili

Advertisement Scroll To Keep Reading

 

Jumapili ya Septemba 18, 2021 Serikali itaweka wazi kilichosainiwa na Mawaziri wa pande mbili za Muungano katika kutatua kero za Tanganyika na Zanzibar.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Ahadi hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumzia mipango ya Taifa leo alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dodoma.

Msigwa amesema siku hiyo atamuita mtaalam ambaye atajibu swali hilo moja kwa moja kutipia mitandao ya kijamii ili Watanzania wajue pande mbili zimesaini kitu gani kwani siyo siri.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililouzwa na mwananchi kwa njia ya simu akitaka kujua vitu gani vimesainiwa na pande mbili katika mkutano wao.

Hivi Karibuni Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aliongoza kikao cha pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano kikilenga kupunguza changamotoza muungano ambazo zimedumu kw amuda mrefu.

“Swali zuri sana hili, lakini naomba nisimalize uhondo tusubiri siku ya Jumapili nitamleta mtaalamu hapa hapa atasimama na kutoa maelezo ya kina nini kimeuznguma na utekelezaji wake utakuwaje,” alisema Msigwa.

Msigwa amesema Tanzania imepania kumaliza migogo ambayo imekuwa ni kero kwa pande zote hivyo wananchi waendelee kuamini kuamini kuwa serikali yao iko kazini na mambo yanaendelea

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.