By Peter Saramba

Chato. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amesema tofauti na miaka iliyotangulia, mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zilikuwa za kipekee kwa Watanzania.

Akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru zinazofikia kilele leo Alhamisi Oktoba 14, 2021 mjini Chato, Waziri Mhagama ametaja maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru kuwa ni miongoni mwa mambo yanayofanya mbio za mwaka huu kuwa za kipekee kwa Watanzania.

Soma zaidi:Miradi ya Sh15.3 bilioni yakataliwa na Mwenge wa Uhuru

Ametaja kitu kingine cha kipekee kuwa, mbio za mwaka huu zinafanyika wakati Taifa likiwa limewapoteza Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

“Tumekimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu huku Taifa likiwa limewapoteza viongozi wakuu wawili; Rais Magufuli na Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa,” amesema Waziri Mhagama

Amesema Mwenge wa Uhuru umekimbizwa mwaka huu muda mfupi baada ya Taifa kupita kwenye  mabadiliko makubwa ya kiuongozi baada ya kifo cha ghafla cha Hayati Magufuli.

Advertisement

“Tunakushukuru na kukupongeza mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa kutuvusha na kutuongoza salama,” amesema Waziri Mhagama

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles