Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Marais wa Kenya na Estonia waahidi kushirikiana kukuza uchumi

Advertisement Scroll To Keep Reading

Rais Uhuru Kenyatta Alhamisi alifanya mazungumzo ya pande mbili na mwenzake wa Estonia Kersti Kaljulaid.

Kaljulaid yuko Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Wakati wa majadiliano, viongozi hao wa nchi mbili walishuhudia kusainiwa kwa mpangokazi wa pande mbili wa ushirikiano juu ya Ushauri wa Kisiasa, Afya na pia kutia saini barua yenye azimio la kimazingira.

Viongozi hao wawili walionesha kuridhika na ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbali mbali haswa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na uvumbuzi ambapo Estonia inasifiwa sana kama mfano mwema duniani.

Uhuru alimshukuru Kaljulaid kwa kuandamana na ujumbe wa ngazi ya juu wa kibiashara kushiriki katika Jukwaa la Biashara kati ya Kenya na Estonia kwa kuzingatia huduma za elektroniki.

Viongozi hao wawili walisisitiza kujitolea kwao kuendelea kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbali mbali kama biashara na uwekezaji na hata mabadiliko ya kidijitali kwa lengo la kuhuisha ukuaji wa uchumi ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kenya.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.