Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

Marais waonyesha mshikamano kipindi kigumu cha mgawanyiko Marekani

Advertisement Scroll To Keep Reading
Biden alisimama bega kwa bega na marais wa zamani Barack Obama na Bill Clinton huko New York City, ambako ndege mbili ziligonga katika jengo la World Trade Center siku iliyokuwa na mwanga wa jua asubuhi miaka 20 iliyopita.

George W. Bush

George W. Bush

Kwa upande wake Rais wa zamani George W. Bush aliungana na Makamu wa Rais Kamala Harris huko Shanksville, Pennsylvania, katika eneo jingine ambapo ndege ya United Airlines namba 93 ilianguka, ambapo watu wote 44 waliokuwa ndani ya ndege walifariki baada ya abiria kujaribu kukabiliana wa watekaji nyara wa ndege hiyo.

Advertisement Scroll To Keep Reading
Makamu wa Rais Kamala Harris

Makamu wa Rais Kamala Harris

Biden hakutoa hotuba katika matukio matatu ya maadhimisho aliposhiriki, ikiwemo lile la Shanksville na Wizara ya Ulinzi. Lakini akiongea na waandishi wa habari pembeni ya matukio hayo, alisema anahisi ni muhimu kuzuru maeneo yote matatu ya kumbukumbu ya Septemba 11.

Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakishiriki katika hafla ya kuweka shade la maua katika maadhimisho ya miaka 20 ya mashambulizi ya kigaidi huko Wizara ya Ulinzi - Kumbukumbu ya waliokufa eneo la Pentagon mjini Washington, Sept. 11, 2021.

Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakishiriki katika hafla ya kuweka shade la maua katika maadhimisho ya miaka 20 ya mashambulizi ya kigaidi huko Wizara ya Ulinzi – Kumbukumbu ya waliokufa eneo la Pentagon mjini Washington, Sept. 11, 2021.

“Kumbukumbu hizi ni muhimu kwelikweli,” amesema. “Lakini pia zina machungu makubwa kwa watu walioathirika na matukio yake, kwa sababu yanarejesha hisia walizopitia pale walipopokea simu, yanarejesha huzuni wakati ule walipopata habari za shambulizi, haijalishi miaka mingapi imepita.”

Ujumbe wake mkuu, alioutoa katika maelezo yake yaliyokuwa yamerekodiwa na kutolewa katika mkesha wa maadhimisho hayo, yalijikita katika suala la umuhimu wa kuwepo umoja wakati migawanyiko ya kisiasa ikiongezeka.

Akiweka mkazo katika kueleza zaidi juu ya hilo, alisema kuwa wakati aliposimama katika Idara ya Zimamoto ya Kujitolea Shanksville, alipiga picha na waliohudhuria ambao walikuwa wamevaa kofia kuonyesha uungaji mkono wao kwa Rais Donald Trump.

“Hivi tutaendelea kwa miaka minne, mitano, sita, kumi kuonyesha kuwa demokrasia inaweza kuwepo au la?” alisema.

‘Umoja ni kitu cha lazima’

Wito wake kwa umoja wa kitaifa ulirejewa na Harris huko Shanksville mapema siku hiyo.

“Katika siku zilizofuatia tukio la Septemba 11, 2001, sote tulikumbushwa kuwa umoja unawezekana kufikiwa Marekani,” amesema.

“Tulikumbushwa, pia, kuwa umoja ni kitu cha lazima Marekani. Ni muhimu kwa ajili ya mafanikio yetu ya pamoja, usalama wa taifa letu, na pia mfano wetu kwa ulimwengu.”

Advertisement Scroll To Keep Reading

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.