Mkondo mwingine wa mazungumzo kati ya Iran na mataifa yenye nguvu, juu ya kuyafufua makubaliano ya mwaka 2015 kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo, yataanza hivi karibuni. 

Hayo ameyasema mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Qatar. 

Afisa huyo alikuwa akimaanisha mazungumzo kupitia mawakala baina ya Marekani na Iran ambayo yalianza mwezi Aprili mjini Vienna, lakini yakaahirishwa siku mbili baadaye kufuatia ushindi wa mwanasiasa mwenye msimamo mkali Ibrahim Raisi kuwa rais mpya wa Iran. 

Tangu aingie madarakani, Iran inasema inazifanyia tathmini awamu za awali za mazungumzo hayo. 

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliiondoa nchi yake katika makubaliano ya mwaka 2015, lakini mrithi wake Joe Biden anataka kuirejesha, ingawa bado serikali yake inatofautiana na Iran juu ya vigezo muhimu.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles