AfricaSwahili News

Mbunge wa Babati Vijijini kutoa Mabati 110 shule ya Msingi

Na John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini (CCM) Mheshimiwa Daniel Sillo ameahidi kutoa mabati 110  kukamilisha ujenzi wa shule shikizi ya msingi Datar iliyopo kata ya Ufana wilayani hapo.

Amesema mabati hayo atayatoa kutoka kwenye fedha za mfuko wa jimbo 2021/2022 ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu na kuwapunguzia msongamano.

Sillo  aliitembelea shule hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea ikiwa ni mwendelezo wa kuzitembelea shule mbalimbali na kutoa misaada ambapo ameshatoa mifuko ya saruji kwenye shule zilizopo jimboni kwake pamoja na mashine za kutolea nakala (photocopy) kwa baadhi ya shule za Sekondari.

Mheshimiwa Sillo  amefanya Ziara kwa Kata ya Secheda na Ufana ikiwa ni muendeleo wa Ziara yake kwa kata zote 25 zilizomo ndani ya Jimbo hilo katika kuwashukuru, kuwasikiliza wananchi, kutatua kero zinazowakabili sambamba na kuwahamasiha juu ya utendaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Katika ziara hiyo Mhe Mbunge ameambata na Viongozi wa chama cha Mapinduzi pamoja  wataalamu kutoka Idara mbalimbali  ili kuweza kubainisha changamoto zinazowakabili wananchi na kuzipatia majawabu ya papo kwa hapo.

Akizungumza katika Ziara hiyo Mhe Mbunge amewahimiza wananchi wa kata hizo juu ya kuwa wamoja na kushirikiana katika kutatua changamoto za kata hiyo sambamba na kuwataka kupokea fedha za maendeleo zinazotolewa na serikali ili kuruhusu huduma za kijamii kuendelea.

Kwa upande wake katibu wa Umoja wa  Vijana wa Chama cha Mapinduzi Babati Vijijini George Sanka  amewataka viongozi wa vijiji  kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika maeneo yao na kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo huku akisisitiza ushirikiano na umoja.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.