More
  - Advertisement -

  Meli ya ‘kijasusi’ ya Iran yashambuliwa kwa makombora Bahari ya Shamu

  -

  - Ad Keep reading below -

  Meli ya mizigo ya Iran imeshambuliwa kwa mlipuko ikiwa imetia nanga katika pwani ya Bahari ya Shamu nchini Yemen. Meli hiyo inadaiwa kutumiwa na kitengo maalum cha jeshi la Iran kwa kazi za kijasusi.

  Wizara ya mambo ya nje ya Iran imethibitisha shambulia hilo.

  - Ad Keep reading below -

  Mlipuko huo uliolenga meli hiyo kwa jina Saviz Jumanne haukusababisha majeruhi yoyote na shambulio hilo linafanyiwa uchunguzi, msemaji wa wizara hiyo amesema.

  “Ilikuwa ni meli ya kiraia iliyowekwa hapo kulinda eneo hilo dhidi ya maharamia,” aliongeza.

  - Ad Keep reading below -

  Gazeti la New York Times limeripoti kuwa Israel imeiambia Marekani kwamba imevamia meli ya Saviz.

  Maafisa wa Israeli hawajasema lolote hadi sasa lakini ndio shambulizi la hivi karibuni kabisa kutekelezwa na Israeli dhidi ya meli za Iran ambapo nchi hizo mbili zinatupiana lawama.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Iran Saeed Khatibzadeh amesema mlipuko huo uliovamia meli ya Saviz takriban saa 06:00 saa za eneo, Jumanne ulisababisha “uharibifu kidogo”.

  “Uchunguzi wa kiufundi na chanzo cha mlipuko huo unaendelea na nchi yetu itachukua hatua zote stahiki kupitia mashirika ya kimataifa,” aliongeza.

  - Ad Keep reading below -

  Bwana Khatibzadeh alisema kuwa meli ya Saviz “haikuwa ya kijeshi”, na ilikuwa inasaidia “kutoa usalama katika ukanda huo kukabiliana na uharamia”.

  Katika taarifa iliyotolewa na komanda wa Marekani imesema kuwa “hakuna mwanajeshi yeyote wa Marekani aliyehusika kwenye tukio hilo”.

  Maafisa wa Iran hawajamlaumu yoyote kwa tukio hilo lakini gazeti la New York Times limemnukuu afisa wa Marekani ambaye hakutajwa akisema kwamba Israel ilikuwa imeiarifu Marekani kwamba wanajeshi wake wamevamia meli hiyo.

  Afisa huyo alisema meli ya Saviz iliharibiwa eneo la chini ya maji na kwamba Israel ilikuwa imevamia meli hiyo “ikilipiza kisasi kutokana na mashambulizi ya awali yaliyotekelezwa na meli za Iran dhidi ya meli za Israeli”.

  Waziri wa ulinzi wa Israeli Benny Gantz amekataa kusema lolote lakini amenukuliwa na gazeti la Maariv akisema: “Tuna mifumo ya mashambulizi inayofanyakazi saa 24, siku 365 kwa mwaka na pia wako tayari kuchukua hatua katika eneo lolote lile bila kujali umbali.”

  Jumanne, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikiambia chama cha Likud kuwa Israel “lazima iendelee kujilinda dhidi ya uchokozi wa Iran katika eneo hilo”.The US military’s Central Command said in a statement that “no US forces were involved in the incident”.

  Meli kadhaa zimeharibiwa hivi karibuni katika kile kinachodaiwa kuwa makabiliano kati ya Israeli na Iran.

  Bwana Netanyahu ameilaumu Iran katika mlipuko uliosababisha shimo kwenye chombo cha Israeli katika ghuba ya Oman mnamo Februari 26 – madai ambayo yamekanushwa na serikali.

  Chombo cha habari cha Iran, wakati huo huo kimeripoti kuwa Israeli ilikuwa inashukiwa kutekeleza mlipuko uliosababisha moto katika meli ya Iran kwenye Bahari ya Mediteranea Machi 10.

  Na Machi 25, meli ya Israeli ya kubeba mizigo ilipigwa na kombora katika Bahari ya Arabia kwenye shambulizi jingine ambapo Iran inashukiwa kulitekeleza, maafisa wa usalama 

  Meli Saviz – ina milikiwa na Iran na iliingia kusini mwa Bahari ya Shamu mwishoni mwa mwaka 2016 na kutia nanga kwenye maji ya kimataifa karibu na mlango bahari wa Bab al-Mandab katika kipindi cha miaka mitatu unusu iliyopit

  Mlango bahari wenye upana wa kilomita 29 unaunganisha mfereji wa Suez na Bahari ya Shamu katika ghuba ya Aden na Bahari ya Arabia.

  Meli zinazobeba takriban mapipa milioni ya sita ya mafuta ghafi na bidhaa za petroli na tani milioni kadhaa za mizigo hupita kwenye njia hiyo kila siku.

  Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unapigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen, mwaka 2018 ulidai kuwa meli Saviz ni meli ya kijeshi ya Iran inayotumiwa kwa shughuli za kijasusi dhidi ya meli zingine na pia kuratiibu mashambulizi katika Bahari nyekundu na kundi la wanamgambo wa Houthi lenye kuungwa mkono na Iran.

  Hata hivyo, Iran imekanusha mara kadhaa kushirikiana na kundi la Houthi. Aidha, wanamgambo hao pia walikanusha taarifa za kushambulia meli zingine za kibiashara katika Bahari ya Shamu.

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Vivo V21 5G India Launch Soon Likely, Gets BIS Certification

  Vivo V21 5G may soon be launched in India as the smartphone has been spotted on the Bureau of Indian Standard (BIS)...

  Do not pressure staff to return to office, Varadkar tells employers

  Employers should not pressure their staff to return to offices or workplaces as Covid-19 restrictions ease, the Tánaiste has warned. Leo Varadkar said there...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -