Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

Mfanyakazi wa Benki akatwa mkono na muweke kisa wivu wa mapenzi

Advertisement Scroll To Keep Reading

By Suzy Butondo

Shinyanga. Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,  Debora Rwekwama (34) mkazi wa Bushushu mjini Shinyanga amekatwa mkono wa kushoto na mumewe, Jacob Mwajenga (35) ikidaiwa ni kutokana  na wivu wa mapenzi.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Kamanda wa  polisi mkoani Shinyanga,  George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2021 mtaa wa Bushushu manispaa ya Shinyanga.

Amesema mwanaume huyo alimkata mkono Debora baada ya mwanamke huyo kuzimia kwa kipigo.

“Inadaiwa mwanaume huyo mchana alikwenda  benki hakumkuta mkewe lakini alikuta mkoba wake katika ofisi   na aliporejea alitaka kuanzisha vurugu lakini wakamshauri ugomvi wao wakaumalize nyumbani.”

“Walipofika nyumbani waliendelea na ugomvi na alimpiga sana mkewe hadi akazirai. Alichukua kisu na kumkata mkono inaonekana zilitoka damu nyingi. Mkewe akiwa amezimia huyu mwanaume alimbeba na kumpakia kwenye gari  na kwenda wilayani Kahama katika kituo cha polisi na kuripoti kuwa  amepata ajali. Kwa sababu Debora  alikuwa hawezi kuongea  hawakumhoji huhu mwanaume walimpa PF 3 ili aweze  kutibiwa lakini hawakujua kama ni mke wake.”

“Alipomfikisha hospitali madaktari walifanya uchunguzi wao na kugundua kuwa hajapata ajali bali amepigwa na walitoa taarifa polisi wilaya ya Kahama ambao walimkamata mhusika ambaye shughuli yake ni kuongoza watalii huko Arusha na kutokana na changamoto ya corona alikuwa nyumbani tu,  nadhani ndio wivu ulipoanzia hapo, “amesema Kyando.

Advertisement

Amesema Debora amelazwa  hospitali ya Wilaya ya Kahama na hali yake ni mbaya, ” tunamshikilia mtuhumiwa  kwa ajili ya uchunguzi zaidi.”

This article Belongs to

News Source link

Advertisement Scroll To Keep Reading

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.