Waandamanaji wanaounga mkono jeshi la Sudan wameendelea na maandamano kwa siku ya tatu mfululizo, wakiongeza joto la shinikizo ambalo Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ametaja kama mgogoro mbaya na hatari sana kwa mabadiliko ya utawala wa nchi hiyo.

Waandamanaji wamekusanyika nje ya makao makuu ya rais mjini Khartoum, wakiitaka serikali ya mpito kuvunjiliwa mbali kwa madai kwamba imekosa kutekeleza wajibu wake kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya raia wa Sudan.

Maandamano yanatokea wakati siasa za Sudan zinajaribu kujitoa katika mgawanyiko uliotokea baada ya kuangushwa kwa utawala wa Omar al-Bashir.

Waandamanaji wanaounga mkono serikali nao wanapanga kuandamana kesho Jumanne.

Tagged in: