More
  - Advertisement -

  Milioni 311.9 kutumika kuchonga Barabara hifadhi za taifa Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe

  -

  - Ad Keep reading below -

  Serikali imetenga shilingi  milioni 311.9 zitakazotumika  kuchonga Barabara yenye urefu wa kilometa 20 katika hifadhi ya Taifa  Rumanyika karagwe na kilometa 51 katika  Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa katika mwaka wa fedha 2020/2021.

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Kyerwa Mhe. Innocent Sebba  Bilakwate (CCM)  ambaye alihoji kuhusu mpango wa  Serikali  wa kuweka miundombinu mizuri ya Barabara katika hifadhi hizo Ili kuvutia watalii.

  - Ad Keep reading below -

  Akijibu Swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro  ,Mhe. Masanja ameeleza kuwa hifadhi za Taifa za Ibanda Kyerwa na Rumanyika karagwe  zilianzishwa kupitia tangazo la Serikali Na 509 na 510 la tarehe 5/7/2019 .

  ALSO READ  Okorocha’s ALGON chairmen make u-turn on forceful take over of offices

  Amesema hifadhi hizo zilitokana na kupandishwa hadhi kwa yaliyokuwa mapori ya akiba ya Ibanda na Rumanyika .

  - Ad Keep reading below -

  “Ili  kuwezesha hifadhi hifadhi hizo kufikika kwa urahisi Serikali kupitia  TANROADS na TARURA iliyokuwa ikitengeneza Barabara mbalimbali zinazorahisha kufika kwa watalii katika hifadhi hizo , Barabara hizo ni pamoja Mgamkorongo iliyopo wilaya ya korogwe hadi murongo wilayani Kyerwa yenye urefu wa kilometa 112 ambayo inafanyiwa   matengenezo na TANROADS kila mwaka na imewekwa  katika mpango wa Kujengwa kwa kiwango cha lami katika mwaka wa fedha 2020/2021” Amesisitiza Mhe.Mary Masanja.

  ALSO READ  Ex-Tahidi High Star Offers Lessons to Struggling Celebrities

  Aidha, amesema jitihada hizo za kuboresha miundombinu ya Barabara katika hifadhi ya Taifa Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe na maeneo mengine yote ya hifadhi zitasaidia kuweka Mazingira mazuri  yatakayowezesha hifadhi hizo kutembelewa na watalii wengi wa maeneo ya karibu pamoja na wageni kutoka nchi jirani.

  Kuhusu ulinzi wa maeneo hayo  ameeleza  kuwa wizara imekuwa ikiyaanisha maeneo yote na kuweka mipaka.

  ALSO READ  Konshisha killings: HURIWA warns COAS, Attahiru against human rights abuse

  ” Katika hifadhi ya Ibanda Kyerwa na Rumanyika tulifanya tathmini baada ya  wataalamu wetu kuainisha mipaka, utekelezaji wake tunaendelea nao kwa kuandaa Mazingira ya kuwapeleka wataalamu kwa ajili ya gharama za uthamini na kuanisha maeneo ambayo yanachangamoto za uhifadhi ” Amesisitiza.

  - Ad Keep reading below -

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Chicago to Release Video of Cop Fatally Shooting 13-Year-Old | Illinois News

  By DON BABWIN, Associated PressCHICAGO (AP) — Body camera footage of a Chicago police officer fatally shooting a 13-year-old boy last month will be...

  Mother sues Nsambya hospital over negligence, seeks Shs 400m

  Rose Namara accuses Nsambya hospital of medical negligence ...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -