Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel ametoa rai kwa watendaji wa umma kuwasumbia wawekezaji kwa kutaka rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na maendeleo.

ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampuni ya usafirishaji wa mizigo kutoka China,Dubai kuja Tanzania ya Silent Ocean iliyofanyika Mkoani Mwanza katika  ofisi ya GSM .

 Mkuu wa Mkoa amewakaribisha wawekezaji na Wafanyabiashara mbalimbali kuja kuwekeza katika mkoa wa Mwaza katika sekta ya Kilimo ,Biashara, Utalii, Ujenzi, Elimu, Ufugaji, na Afya.

Mhandisi Gabriel amesema ofisi yake ipo tayari kuwapokea wawekezaji na wafanyabiashara wanaokuja kuwekeza na kuahidi kuwapatia ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuwapatia maeneo ya uwekezaji.

Hata hivyo aliongeza kuwa chini ya uongozi wake hawatavumilia vitendo vyote vya rushwa na unyanyasaji kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji na endapo wakikutana na changamoto hiyo taarifa ifike ofisini kwake.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo ,Mohamed soloka amesema kuwa wameamua kufungua tawi mkoani Mwanza kutokana na uhitaji mkubwa wa wafanyabiashara na uungaji mkono wa serikali.

Nae mkuu wa Masoko na mauzo, Mohamed Kamilagwa amesema itawapunguzia Wafanyabiashara usumbufu wa kusafirisha biashara kutoka China na Dubai kuja Mwanza hivyo kunufaika kiuchumi.

“Mteja atasaidiwa kupunguza usumbufu wa kuulizia mzigo kutoka Dar es salaam lakini wale wajasilimiamali  tulionao itawarahisishia kuwapunguzia gharama za kusafirisha ,usumbufu wa kuuliza na kuokoa mda ,”alisema Kamilagwa.

Hata hivyo kwa upande wa serikali amesema kuwa hii inaenda kuongeza pato la serikali kupitia kodi kutokana na endapo wajasiliamali wataongezeka .

Mfanyabiashara katika jiji la Mwanza, Betty Mgema  alisema kampuni hilyo ltawasaidia wao katika kusafirisha mizigo kutoka China na Dubai kuja Mwanza  kwani itatupunguzia gharama ya kusafiri na muda.

Pia alitoa shukrani kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa kuwahakikishia ushirikiano Wafanyabiashara kwa kuwapatia maeneo ya biashara na kuwalinda dhidi ya unyanyasaji.

Nae mfanyabiashara Juliana Masalu alisema hapo awali walikuwa wanapata usumbufu wa kusafili kwa ndege kutoka Mwanza kwenda Dar es salaam kufuata mizigo lakini kutokana na ujio wa kampuni hilo litawasaidia kupokea mizigo Mwanza .

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles