Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA nchini Samweli Mwela, amesema kuwa katika kuelekea na kuufikia ulimwengu wa kidijitali, hakuna mwananchi yeyote atakayeachwa nyuma, na kusisitiza kwamba matumizi ya TEHAMA yatumike kujiletea maendeleo na si vinginevyo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba Mosi, 2021, kwenye kipindi cha #DriveShow cha East Africa Radio, kuelekea Oktoba 20 ha 22 siku ambazo litafanyika kongamano pamoja na utoaji wa Tuzo za TAHAMA #ICTAwards2021 litakalofanyika mkoani Arusha.

“Tutahakikisha hakuna Mtanzania atakayeachwa nyuma katika masuala ya kidijitali, kwa wabunifu tutakuwa na maonyesho ya makampuni yanayoanza, na watu 10 watakokuwa wanafanya vizuri watashiriki bure,” amesema Bw. Mwela.

Aisha, ameongeza kuwa, “Katika kongamano litakaloanza Oktoba 20-22 mkoani Arusha tunawakarinbisha Waandishi wa Habari na wanafunzi kushiriki ili waweze kuona na kujifunza teknolojia, na kujenga moyo kwamba TEHAMA ni kitu kizuri, niwakaribishe pia wataalam wa TEHAMA wajitokeze kujisajili na waweze kupewa vyeti”.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles