AfricaSwahili News

Mkuu wa zamani wa ujasusiwa Israel afichua oparesheni za Mossad dhidi ya Iran

Mkuu anayemaliza muda wake wa shirika la ujasusi la Israeli Mossad ametoa ufichuzi wa oparesheni za Mossad dhidi ya Iran katika mahojiano ya kipekee .

Yossi Cohen alitoa maelezo juu ya wizi wa stakabadhi za nyuklia za Iran.

Uvamizi wa ghala mnamo 2018 ulichukua maelfu ya nyaraka kutoka nchini humo kwenda Israeli.

Alidokeza pia kuhusika kwa Israeli katika uharibifu wa kituo cha nyuklia cha Irani huko Natanz, na mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia.

Bwana Cohen alistaafu kama mkuu wa Mossad wiki iliyopita.

Alizungumza na mwandishi wa habari Ilan Dayan kwenye kipindi maalum cha runinga cha Uvda cha Channel 12, kilichopeperushwa Israeli Alhamisi usiku.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alimteua Bwana Cohen kama mkuu wa Mossad mwishoni mwa mwaka 2015. Alijiunga na shirika hilo mnamo 1982 baada ya kusoma katika chuo kikuu huko London, na aliambia kipindi hicho kwamba alikuwa na “mamia” ya pasipoti katika kipindi chote cha kazi yake.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button