More
  - Advertisement -

  Mo Dewji miongoni mwa matajiri 18 wenye pesa zaidi Afrika

  -

  - Ad Keep reading below -

  Afrika yajivunia mabilionea 18 utajiri wao wote kwa ujumla ukiwa dola bilioni 74, kulingana orodha mpya iliyotolewa na jarida mambo ya kibiashara na utajiri la Forbes.

  Kwa mujibu wa orodho iliyotolewa jana Jumanne, Aliko Dangote wa Nigeria anaendelea kuongoza kwa utajiri kwa mwaka wa 10 mfululizo huku utajiri wake ukiwa dola bilioni 11.6. Hata hivyo, Dangote ni wa 190 katika orodha ya matajiri wa dunia nzima.

  - Ad Keep reading below -

  Barani Afrika, Dangote alifuatwa na Nassef Sawiris wa Misri utajiri wake ukiwa ni dola bilioni 8.5, Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini akiwa na utajiri wa dola bilioni 8, Johann Rupert wa Afrika Kusini akiwa na dola bilioni 7.2 huku Mike Adenuga wa Nigeria thamani yake ikiwa ni dola bilioni 6.3.

  Kwa upande wa Afrika Mashariki, Mtanzania Mohammed Dewji pekee ndiye aliyeingia katika orodha hiyo.

  - Ad Keep reading below -

  Ingawa idadi ya matajiri hao katika jarida la Forbes iliongezeka kote duniani huku ikiweka rekodi kwa kuongeza watu wapya 493, idadi ya mabilionea wa Afrika ilipungua kidogo ikilinganishwa na mwaka 2020 ilipokuwa 20.

  ALSO READ  Askari wanaodaiwa kumuua mwanachama wa ACT wakamatwa
  ALSO READ  Serikali yadhamiria kuwawezesha vijana kupitia programu ya mafunzo ya Ujasiriamali

  Mabilionea 18 wa Afrika wanatoka mataifa mbalimbali kama vile Afrika Kusini na Misri zikiwa na matajiri watano kila mmoja, Nigeria ikiwa na matajiri watatu, Morocco matajiri wawili, Zimbambwe, Tanzania na Algeria wakiwa na tajiri mmoja kila mmoja.

  1. Aliko Dangote – Nigeria – ana thamani ya $11.6b

  2. Nassef Sawiris – Misri – ana thamani ya $8.5b

  - Ad Keep reading below -

  3. Nicky Oppenheimer – Afrika Kusini – thamani ya $8b

  4. Johann Rupert – Afrika Kusini – ana thamani ya $7.2b

  5. Mike Adenuga – Nigeria – ana thamani ya $6.3b

  6. Abdulsamad Rabiu – Nigeria – ana thamani ya $ 5.5b

  7. Issad Rebrad – Algeria – ana thamani ya $4.8b

  8. Naguib Sawiris – Misri – ana thamani ya $3.2b

  9. Patrice Motsepe – Afrika Kusini – ana thamani ya $ 3b

  10. Koos Bekker – Afrika Kusini – ana thamani ya $2.8b

  11. Mohamed Mansour – Misri – $2.5b

  ALSO READ  Jobs bloodbath continues at N Cape mine amid state capture hearings

  12. Aziz Akhannouch – Morocco – $2.0b

  ALSO READ  Varadkar hits out at Sinn Féin’s handling of ‘racist and homophobic’ remarks

  13. Mohammed Dewji – Tanzania – $1.6b

  14. Youssef Mansour – Misri – $1.5b

  15. Othman Benjeloun – Morocco – $1.3b

  16. Michiel Le Roux – Afrika Kusini – $1.2b

  17. Strive Masiyiwa – Zimbabwe – $1.2b

  18. Yaseen Mansour – Misri – $1.1b

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  VIDEO | Christina Shusho – Shusha Nyavu

  https://www.youtube.com/watch?v=eOGKpXVSkDU ...

  Masanja alivyogeuka mbogo kwa waandishi kwa kuzimiwa taa akiwaombea waache umbea (+ Video)

  Leo @mkandamizajii alikuwa Mbagala katika kutoa misaada kwa akina mama ntilie hasa vifaa vya kujikinga na CORONA kama Sanitizer, Barakoa, Ndoo za kunawia maji kwa kuungana...

  M&S take legal action against Aldi over Colin the Caterpillar trademark

  Marks and Spencer has launched legal action against Aldi over a claim that the discount supermarket is infringing the trademark of its Colin...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -