Morphine na cocaine iliyofichwa kwenye vifungo vya kitenge vilinaswa Alhamisi katika uwanja wa ndege ya Jomo Kenyatta,JKIA nchini Kenya .

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti amesema kasha la dawa hizo za kulevya zilizofichwa katika vifurushi viwili zilinaswa kufuatia habari walizopokea awali.

“Moja ya shehena ambazo zilikuwa zilipelekwa Australia kutoka Kenya zilitajwa kuwa pete za jadi za Kiafrika,” alisema.

Kinoti alisema mtu wa kawaida angechukulia jozi 168 za vipuli kuwa vipuli kama ilivyoripotiwa .

“… lakini maafisa wa polisi waliokuwa makini waliona kuna zaidi ndani ya kifurushi hicho. Baada ya uchunguzi wa kina, waligundua podari ya manjano iliyofichwa kwa ujanja ndani ya mapambo,” Kinoti alisema.

Kinoti aliendelea kusema kuwa shehena ya pili ilikuwa imetajwa kuwa nguo 12 za vitenge na ilikuwa ikipelekwa Hong Kong.

Wapelelezi wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya walifungua shehena na wakapata nguo 12 vifungo 199 zaidi vilivyotumiwa kuficha dawa hizo.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles