Advertisement Scroll To Keep Reading
Swahili News

Msajili aishauri Chadema kuweka picha ya Rais katika ofisi zao

Advertisement Scroll To Keep Reading

By Peter Elias

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeishauri Chadema kuweka picha ya Rais katika ofisi za viongozi wa chama hicho kwa sababu hiyo ni taasisi ya umma.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza wakati wakifanya ukaguzi wa chama hicho katika utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Amesema ofisi za vyama vya siasa ni ofisi za umma hivyo ni vizuri wakaendeleza utamaduni wa kuwa na picha ya Rais kwenye taasisi za umma.

“Hii ni ofisi ya umma, ni vizuri kukawa na picha ya Rais ukutani, siyo unaweka picha ya katibu mkuu. Huu ni ushauri tumewapa, tutapita Januari kuona kama wamelifanyia kazi,” amesema Nyahoza.

Soma zaidi: Msajili aitisha mkutano kujadili mvutano kati ya polisi, vyama vya siasa

Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amesema Msajili amekuta mambo yamekaa vizuri ndiyo maana akagundua hakuna picha ya Rais.

Advertisement

“Tumempokea Msajili, wamepitia taarifa zote walizozihitaji wamekuta mambo yako vizuri, ni masuala madogo madogo ndiyo yanahitaji kufanyiwa kazi. Kama angekuta mambo makubwa, asingekumbuka kuangalia picha ya Rais,” amesema Mwalimu.

Soma zaidi:Msajili aanza kutembelea ofisi za vyama, aionya AAFP

Ofisi ya Msajili inaendelea na ukaguzi wa vyama vya siasa na leo walikuwa wakikagua Chadema ambapo Nyahoza amesema wamefurahishwa na mfumo mzuri wa uwekaji kumbukumbu za fedha na wana mfumo mzuri wa utawala.

Hata hivyo, amesema wamebaini mapungufu kadhaa ikiwemo uwekaji kumbukumbu kwenye mali za chama na pia wameanza kutumia bajeti ambayo wameiandaa lakini haijaidhinishwa na kamati kuu kama katiba yao inavyotaka.

Imeandikwa na Irene Meena na Peter Elias

This article Belongs to

News Source link

Advertisement Scroll To Keep Reading

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.