By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mfanyabiashara na mwandaaji wa matamasha wa nyimbo za injili, Alex Msama amejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Msama ambaye ni Mkurugenzi wa kamnpuni ya Msama Promotion amejitokeza leo Januari 15, 2021 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, ikiwa zimebaki saa chache kufungwa kwa shughuli hiyo.

Uchukuaji fomu ulianza Januari 10 baada ya kutangazwa nafasi ya uspika kuwa wazi kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge hilo,Job Ndugai Januari 6,2022.

Akizungumza mara baada ya kutoka kuchukua fomu, Msama aliyekuwa amevalia shati la kitenge lenye rangi maua enye rangi ya kijani iliyochanganyika na njano na surali nyeusi, amesema amejitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kugombea Uspika na sio kwa kujaribu bali anaamini kuwa anao uwezo.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema na kuweza kuamka kukamilisha hatua hii ya uchukuaji fomu kuomba nafasi katika chama changu.

“Ni nafasi pekee na historia kubwa katika maisha yangu, na ninajiamini uwezo ninao kwani mbali na kumtegemea Mungu kwa kwa kuwa yeye ndio muweza wa yote pia ninaweza, hivyo nitaijaza fomu hii leoleo na kuirudisha,” amesema Msama.

Advertisement

Kwa mujibu wa Msaidizi Mkuu idara ya Oganaizesheni Solomon Itunda, hadi kufika jana wanachama 66 wamehitokeza kuchukua fomu kuomba kuwania kiti hicho.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles