By Mwandishi Wetu

Abdulrazak Gurnah mwenye asili ya Zanzibar ambaye ni mshindi wa tuzo ya fasihi ya Nobel kwa utunzi wake juu ya ukoloni mamboleo na masuala ya wakimbizi mwenye  amesema tuzo hiyo ni kitu cha umuhimu kwake.

SOMA: Mtanzania ashinda tuzo ya fasihi ya Nobel

Gurnah aliyezaliwa  na kukulia visiwani Zanzibar lakini akakimbilia Uingereza kama mkimbizi mwishoni mwa miaka ya 1960 hakuwahi kuwaza kushinda tuzo hiyo kubwa.

Akizungumza na Azam Tv jana Alhamisi Agosti 7, 2021 amesema amefurahi kuona utunzi wake umechaguliwa hadi kushinda.

“Nimepokea kwa heshima na furaha, sikuwahi kufikiria kuwa kijana kutoka Unguja atapata tuzo, kitu muhimu na kikubwa sana nimefurahi sana kuchagua maandishi yangu na mimi kutoka kwetu, Zanzibar nimefurahi sana.”

“Miaka mingi niliyoandika mambo haya, kusoma kutizima ,  na kufikiri na kujishughulisha na mambo ya watu. Utunzi wa hadithi za watu wetu na watu wa Pwani hadithi za watu wa sehemu zetu waafrika. Mimi nimeondoka miaka mingi iliyopita lakini wazee wangu wamebakia ndugu zangu wamebaki na mimi naenda na kurudi mambo yanakwenda tu,” amesema.

Advertisement

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles