By Mussa Juma

Arusha. Msikiti wa Hidaya uliopo eneo la Olmatejo kata ya Sakina jijini Arusha, umezindua maktaba ya kisasa ya vitabu vya dini na vya elimu ya kawaida, kwa wananchi wa dini zote ili kusaidia vijana ambao wanataka kujiendelea kielimu kujisomea.

Maktaba hiyo, imezinduliwa juzi sambamba na uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa msikiti mpya wa ghorofa nne ambao unatarajiwa kugharimu Sh2.2 bilioni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12 jijini hapa, Sheikh Mkuu wa msikiti huo, Sheikh Omar bin Said Jori amesema uzinduzi wa maktaba hiyo na ramani ya ujenzi wa msikini wa ghorofa nne ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Hidaya ambayo ni mwaka wanne sasa kuadhimishwa.

Sheikh Omari amesema vitabu pamoja ujenzi wa eneo la maktaba hiyo umegharimu zaidi ya sh 7 milioni huku msikini utakajengwa ambao utakuwana ghorofa nne utagharimu zaidi ya Sh2 bilioni.

Amesema kilichowasukuma kufungua maktaba hiyo ni kurejea maagizo ya Mwenyezi Mungu kuwataka na hasa vijana ambao walikuwa wakilazimika kusafiri hadi nje yanchi kutafuta elimu wanaweza sasa kusoma nchini.

“Kufungua maktabahii ni kurejea maagizo ya Mwenyezimungu yakutaka watu kusoma  hivyo, maktaba hiyo itatumiwa na watu wa dini zote kujisomea,” amesem. 

Advertisement

Hata hivyo, Sheikh Omar ameomba wahisani kuendelea kujitokeza kusaidia mradi wa ujenzi wa msikini huo, ambao pia utakuwa na shule ya watoto wadogo ili kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri.

Akizungumzia mradi huo, katika uzinduzi huo, diwani wa kata ya Sakina, Vincent Wilson maarufu kama Fadhili, amesema uzinduzi wa maktaba hiyo ni faraja katika kata yake kwani, sasa utaondoa tatizo la vijana kukaa mitaani bila kazi.

“Lakini pia tunapongeza masjidi Hidaya kwa kuja na mradi wa ujenzi wa msikiti na shule hii itasaidia watoto kusoma kwani katika kata hii hatuna shule,” amesema.

Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya wakazi wa Sakina, wameeleza kuzinduliwa kwa maktaba hiyo ni fursa kwao kujiendeleza kusoma kwani awali kulikuwa hakuna vitabu vingi vya dini katikajiji la Arusha.

Shaaban Juma amesema maktaba hiyo ina juzuuzote za quraani, vitabu vya hadithi,Sunna na maelekezo mbali mbali ya dini ambavyo sio rahisi kuvipata katika maeneo mengine.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles