Mtandao wa YouTube wafuta akaunti za R.Kelly, R.KellyTV & R.KellyVevo

0
2
Kama ilivyokuwa kwa sasa ni kawaida sana kusikia stori mbaya kumhusu mkali wa R& B duniani Robert Kelly alimaarufu R.kelly ambaye siku za hivi karibuni amekutwa na kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono na ikielezwa huenda akapata kifungo cha miaka 20 jela.

Siku ya leo habari nyingine kuhusu R.Kelly ni kwamba mtandaoni wa kuweka maudhui (Content) YouTube umezifungilia mbali akaunti za muziki za R. Kelly (RKellyTV & RKellyVevo) hatua ya kwanza kubwa tangu kutiwa hatiani kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.

Aidha, msanii huyo hatoweza kuzitumia au kufungua akaunti mpya, lakini nyimbo zake kwenye chaneli za watu wengine zitabaki ial katika akaunti zake hazitaonekana tena.