Mamlaka nchini Austria zimeanza kuwakamata wahusika wa kashfa ya ufisadi nchini humo, iliyosababisha kansela Sebastian Kurz kujiuzulu.

Kulingana na gazeti la kila siku la Austria Der Standard na shirika la habari la APA, mtuhumiwa aliyekamatwa alikuwa akichunguzwa kwa madai ya kufuta taarifa kutoka kwenye mfumo wa kutunzia taarifa wa kompyuta yake muda mfupi kabla ya kuvamiwa na maafisa.

Mtuhumiwa huyo ni mtathmini wa kura za maoni na ni wa kwanza kukamatwa kufuatia kashfa hiyo ya ufisadi.

Kurz na washirika wake wanadaiwa kutumia fedha za umma kulipia kura bandia ya maoni na na kuvilipa vyombo vya habari ili vichapishe habari nzuri wakati wa uchaguzi wa mwaka 2016, ambao Kurz aliyekuwa waziri wa mambo ya kigeni alikuwa akigombea nafasi ya ukansela kupitia chama cha Peoples, ÖVP.