Swahili News

Muswada wa sheria wa kulinda haki ya wanawake kutoa mimba wakwama kwenye baraza la Seneti la Marekani

Katika baraza la Seneti ambalo limegawanyika kulingana na misimamo ya kisiasa, lenye Wademocrats 50 na Warepublican 50, karibu Wademocrats wote waliunga mkono muswada huo unaolinda haki ya wanawake kuondoa mimba, huku Warepublican wote wakiupinga. Muswada huo haukupitishwa kwa kura 51 dhidi ya 49.

Wademocrats wameshindwa kupata kura za kutosha ili kuondoa utaratibu wa kura 60 zinazohitajika ili muswada wa sheria upitishwe.

Muswada huo ulifikishwa Jumatano kwenye kikao cha baraza la Seneti na kiongozi wa walio wengi Mdemocrat Chuck Schumer baada ya maoni ya jaji mmoja wa mahakama ya juu yaliyovuja wiki iliyopita, ambayo yalionyesha kuwa majaji watano wenye msimamo wa kihafidhina kati ya tisa , wanaunga mkono kubatilishwa kwa haki ya kikatiba ya karibu miongo mitano inayowaruhusu wanawake kuondoa mimba.

JOIN US ON TELEGRAM

Related Articles

Back to top button
Muhabarishaji News We would like to show you notifications for the latest news and updates.
Dismiss
Allow Notifications

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker