AfricaSwahili News

Mvua kubwa nchini Pakistan

Watu wanne wakiwemo watoto wawili wamepoteza maisha na wegine watatu wamejeruhiwa katika majanga na ajali zilizosababishwa na mvua kubwa katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa nchini Pakistan.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa ya Khyber Pakhtunkhwa, mvua kubwa imesababisha mafuriko katika mkoa wa Karak na Upper Dir.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani, nyumba katika maeneo yaliyotajwa zimeharibiwa na ardhi nyingi za kilimo zimefurika.

Usafiri pia umesitishwa katika miji ya Gangshal na Sheringal kwa sababu ya mafuriko, wakati nyumba nyingi na biashara zikiwa zimefurika katika mkoa wa Swat.

 

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.