AfricaSwahili News

Mwanafunzi ampiga msumari mkuu wa shule kisa kudaiwa ada

Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika shule ya Sekondari Ainamoi iliyoko Kaunti ya Kericho, Kenya anatafutwa na Polisi kwa kumpigilia msumali wa inchi nne Mkuu wake wa shule

Mwanafunzi huyo alizuiwa kuingia darasani akitakiwa kwanza alipe ada aliyokuwa anadaiwa ambayo ni takriban Tsh. 150,000, ambapo imedaiwa Mwanafunzi aliomba muda zaidi wa kulipa kiasi hicho

Baada ya kutoelewana Mwanafunzi alimvizia Mkuu wa Shule na kumgongelea msumari wa inchi nne kichwani na kwa sasa Mwalimu yupo hospitali kwa matibabu

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button