AfricaSwahili News

Mwanamitindo wa Marekani aomba msamaha kwa kuwadhalilisha watu mtandaoni

 

Chrissy Teigen ameomba msamaha kwa kuwadhalilisha watu kadhaa kwenye Twitter.

Teigen alichapisha msururu wa ujumbe kwenye Twitter mwezi Mei kumuomba radhi mtangazaji wa runinga Courtney Stodden, ambaye alimtuhumu kwa unyanyasaji.

Stodden alikubali msamaha lakini akasema huenda ni jaribio la kusafisha sifa ya Teigen.

Alisema hakuwa akitafuta huruma, na kuongeza kuwa “ameabadilikana sio mtu wa kuandika vitu hivyo vya kutisha” baada ya kuolewa, kupata watoto na kutafuta matibabu.

“Sisi sote ni ztunapitia kipindi kigumu maishani,” Teigen aliandika. “Sitaomba msamaha wenu, ila naomba uvumilivu wenu.”

Mwaka 2011 Teigen, ambaye alikua na miaka 25 wakati, alipotuma ujumbe huo kwa Stodden aliyekuwa na miaka16 akimtaka kujitoa uhai.

Wakti huo Stodden alijizolea umaarufu kama bibi arusi wa mwigizaji Doug Hutchison, ambaye alikuwa na umri wa miaka 50 wakati walioa.

Chrissy Teigen ambaye ni mwanamitindo na mwandishi wa Merekani ana wafuasi milioni 35 kwenye mtandao wa Instagram na wafuasi milioni 13.5 kwenye Twitter.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.