Mwanamuziki maarufu wa Zambia Slapdee amejiondoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumkosoa kwa kufanya maonesho ya muziki kwa chama kilichokuwa madarakani.

Chama hicho cha Patriotic Front kilishindwa uchaguzi na hivyo kundoka madarakani mwezi Agosti.

Slapde, ambaye jina lake halisi ni Mwila Musonda, awali alitetea maamuzi yake ya kufanya maonesho kwa ajili ya maofisa kama biashara lakini inaoneka iliathiri muziki wake.

Kufuatiwa kuchaguliwa Afrimma kushiriki kuwania tuzo, Wazambia walihamasisha watu watu mtandaoni kumpigia kura mwanamuziki wa Afrika Kusini Cassper Nyovest katika kipengele alichokuwa anawania cha mwanamuziki bora wa kiume kusini mwa Afrika ambapo kulikuwa na mshiriki wa Zimbabwe Jah Prayzah naTha Dogg kutoka Namibia na wengine.

Kampeni za kumpinga Slapdee na kumuunga mkono Cassper Nyovest zilizua gumzo mtandaoni.

Mwanamuziki wa Afrika kusini aliandika kwenye twitter “kwanini anazungumziwa Zambia?” alafu akasema “Ni sawa Zambia, hii ni biashara tu”

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles