Mwanariadha Agnes Tirop, aliyeiwakilisha Kenya katika mbio za mita 5000 katika Olimpiki amekutwa amefariki nyumbani.

Mwakilishi wa wanawake wa Kenya katika mbio za mita 5,000 katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo Agnes Tirop ameaga dunia Jumatano, Oktoba 13, nyumbani kwake huko Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Shirikisho la Riadha nchini Kenya AK limetuma salamu za rambi rambi kufuatia taarifa za kifo cha mwanariadha huyo ambaye ni mshindi wa medali ya shaba duniani katika mbio za mita 10,000.

Mwezi uliopita mwanariadha huyo alivunja rekodi ya wanawake katika mbio za kilomita 10,000 katika mashindano ya Road to Records Race nchini Ujerumani

Alishinda pia mashindano ya nyika ya Afrika mnamo 2014 huko Kampala, Uganda na vile vile Mashindano ya Dunia ya nyika kwa Vijana Duniani mnamo 2013 huko Bydgoszcz, Poland.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles