Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Mwanariadha wa Belarus ajisalimisha ubalozi wa Poland Jijini Tokyo

Advertisement Scroll To Keep Reading

Mwanariadha wa Belarus, Krystsina Tsimanouskaya ameonekana ubalozi wa Poland Jijini Tokyo leo ambako amejisalimisha kuepuka kurudishwa kwao kufuatia kuingia kwenye mgogoro na viongozi wa timu yake ya Olimpiki.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Serikali ya Japan imesema Tsimanouskaya yu salama baada ya kulalamika viongozi wa timu yake ya Olimpiki walimpeleka Uwanja wa Ndege wa Haneda Jijini Tokyo ili kumrejesha nyumbani Jumapili jioni baada ya kutofautiana na makocha.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan amesema wanawasiliana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki nan a Waandaji, Jiji la Tokyo juu ya kumsaidia mwanamichezo huyo.

Krystsina aliwashutumu makocha wa Belarus kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba walimlazimisha kukimbia 4×400 relay licha ya kwamba hakuwahi kukimbia kabla. 

Krystsina ambaye leo anatarajiwa kukimbia mbio za mita 200, amesema anahofia usalama wake akirejea Belarus na ataomba msaada wa Ubalozi wa Austria Jijini Tokyo.  

Krystsina alikimbia mbio za mita 100 Ijumaa na kumaliza nafasi ya nne, ambazo alishinda Mnigeria, Blessing Okagbare, ambaye siku moja baadaye alisimamishwa baada ya vipimo kuonyesha mushkeli kwenye hormone zake. 

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.