AfricaSwahili News

Mwanasiasa aomba radhi kwa kumpiga ngumi mporaji Afrika Kusini

Kiongozi wa mkoa wa KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini ameomba radhi kwa kumpiga ngumi mporaji katika jaribio la kumfanya aweke chini bidhaa alizokuwa ameiba katika bohari moja mjini Durban.

Tukio hilo lilinaswa katika kanda ya video na kuanza kusambazwa katika mitandao ya kijami.

“Ijapokuwa hatua ya kumkamata mporaji anayekataa kujisalimisha inakubalika, hatua hiyo inavyotekelezwa inasikitisha sana,” taarifa kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu Sihile Zikalala ilisema.

”Waziri huyo ameomba msamaha kufuatia kitendo hicho. Naamini vurugu hazina nafasi katika jamii na kwa kuzingatia msimamo huo wale wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa sheria hawafuatilii maadili ya nchi yetu”

Serikali sasa inapanga kupeleka wanajeshi 25,000 kukabiliana na maandamano yaliyotibuliwa na kufungwa jela kwa rais wa zamani Jacob Zuma.

Karibu watu 117 wamefariki na wengine zaidi ya 2,000 wametiwa mbaroni katika ghasia hizo mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Afrika Kusini kwa miaka kadhaa.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.