Mwandamanaji wa pili nchini Sudan amefariki baada ya kupigwa kichwani na mkebe wa gesi ya kutoa machozi katika maandamano yanayopinga utawala wa kijeshi, madaktari walisema leo Jumatatu.

Hii inafikisha idadi ya vifo kutoka maandamano ya Jumapili kuwa viwili kutokana na maandamano tangu mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba kufikia vifo 63. Mwandamanaji mwingine alikufa baada ya kuathiriwa shingoni na mkebe wa gesi ya kutoa machozi ilisema kamati kuu ya madaktari wa Sudan ambayo iiko pamoja na vuguvugu la maandamano.

Polisi wa Sudan walisema katika taarifa ya leo Jumatatu, kwamba walikabiliana na uvunjifu wa usalama kwa kutumia nguvu ipasavyo na kwamba kifo kimoja cha raia kilirekodiwa, pamoja na majeruhi wanane. Pia walisema kuwa polisi 22 wamejeruhiwa, na kwamba washukiwa 86 wamekamatwa.

Vikosi vya usalama viliwarushia gesi ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa mshikamano kwenye mji wa Omdurman, ambao umekumbwa na ghasia nyingi katika siku za karibuni.

Tagged in: