Mwenyekiti Bazecha agoma kuandika maelezo Polisi

0
1

By Mariam Mbwana

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema (Bazecha), Hashim Juma anayeshikiliwa na Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za makossa ya kimtandao, amegoma kutoa maelezo ya onyo mbele ya Polisi, akisema atayatoa maelezo hayo mahakamani.

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 5 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, John Mrrema imesema timu ya mawakili wa chama hicho imelitaka Jeshi la Polisi kumpatia dhamana au kumfikisha mahakamani kama sheria inavyotaka.

Soma hapa: Chadema yadai kada wake anashikiliwa na Polisi Zanzibar

Kutokana na hilo, Mrema amesema katika taarifa hiyo liwa chama kimefungua kesi ya maombi ya dhamana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Jeshi la Polisi.

This article Belongs to

News Source link